Uhakiki wa Nafasi ya TEKNOHAMA katika Kukuza Maudhui katika Tamthilia ya Kigogo
Date
2019
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Fasihi ni zao la jamii na hubadilika kila uchao. Uwakilishi wa suala la TEKNOHAMA katika tamthilia za kisasa umechukua mkondo mpya. Hii ni kwa sababu, kutokana na jinsi dunia inavyobadilika ndivyo masuala ya kiteknolojia pia yanavyoathiri fasihi ya sasa na kuipa mguso na taathira mpya. Licha ya uwakilishi wa TEKNOHAMA kuwa na umuhimu katika kukuza fani na maudhui katika fasihi, mchango wake katika tamthilia ya Kigogo haujafanyiwa utafiti, suala linalomchochea mtafiti kulitafiti. Lengo kuu la utafiti huu ni kutathmini mchango wa TEKNOHAMA katika kukuza maudhui katika tamthilia ya Kigogo ya Pauline Kea (2016). Utafiti huu unaongozwa na Nadharia ya Uhalisia. Uteuzi wa sampuli utafanywa kimakusudi na utafiti wenyewe ni wa muundo wa kiudhamano. Mtafiti atasoma ma kala mbali mbali kuhusiana na mada na kisha kuichanganua data kwa njia ya kimaelezo.